Nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi anayeichezea kwa mkopo klabu ya nchini Ujerumani, Borrusia Dortmund amemjibu rais wa klabu ya Atalanta, Antonio Percassi kupitia mtandao wa Twitter mara baada ya rais huyo kutoa majibu juu ya tuhuma zinazoikabili klabu yake kutokana na mashabiki wa klabu hiyo.
Inadaiwa nyota huyo alisikia kelele za mfano wa nyani zikipigwa na mashabiki wa Atalanta kwenye mchezo wa Europa, ambapo Dortmund ilisafiri kuifata Atalanta. Kelele hizo zilitafsiriwa kama ubaguzi wa rangi kwa nyota huyo wakimbagua kutokana na rangi yake, ambapo baadae chama cha soka barani Ulaya kikaahidi kulifatilia suala hilo na kulifanyia uchunguzi.
Rais wa klabu hiyo alijibu tuhuma hizo kwa kusema "Sikusikia chochote juu ya kelele hizo, lakini kama tukio hilo lilitokea kweli basi nichukue fursa hii kumuomba samahani Batshuayi"
Naye Batshuayi alijibu ombi hilo kupitia mtandao wa Twitter kwa kusema "Ni kweli, heri njema kwa mashabiki wako M. Percassi"
MICHY BATSHUAYI ATOA MAJIBU KUHUSU UBAGUZI ALIOFANYIWA
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment