NYOTA MWENGINE KUMFATA GIROUD KLABUNI CHELSEA - Darajani 1905

NYOTA MWENGINE KUMFATA GIROUD KLABUNI CHELSEA

Share This
Chelsea inatajwa kuingia kwenye mipango ya kumnasa nyota mwengine klabuni Arsenal mara baada ya kufanikiwa kumnasa Olivier Giroud kutokea klabuni hapo katika dirisha dogo la mwezi Januari mwaka huu kwa dau la paundi milioni 18. Chelsea inatajwa kuhusishwa na Aaron Ramsey ambaye anaonekana kutopewa kipaumbele klabuni huko.

Chelsea inatajwa kumuwania nyota huyo ambaye mara baada ya kuiongoza Arsenal kupata ushindi wa magoli 3-1 hapo jana usiku dhidi ya Ac Milan alikiri haoni kama Arsenal wanania ya dhati ya kufanya mazungumzo ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kuwa klabuni hapo ambapo mkataba wake wa sasa unaisha kipindi cha kiangazi msimu ujao.

"Hakuna cha kuongezea katika hilo, nahisi (Arsenal) kwa sasa wanahangaika kufanya mazungumzo na wachezaji wengine" alisema nyota huyo ambaye kwa sasa ana miaka 27.

Chelsea inatajwa kuwania saini ya nyota huyo ili kujidhatiti na kujiweka sawa mara baada ya kuwa na msimu mbovu ikitupwa nje ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya lakini pia ikishindwa kutetea taji lake la ligi kuu Uingereza, huku pia ikipewa nafasi ya kumnasa nyota huyo kutokana na kiungo wake, Cesc fabregas nae kutupwa mkono na umri wake huku akikaribia kumaliza mkataba wake klabuni Chelsea.

No comments:

Post a Comment