MARA BAADA YA MVUTANO, CHELSEA YAONYESHWA TAA YA KIJANI - Darajani 1905

MARA BAADA YA MVUTANO, CHELSEA YAONYESHWA TAA YA KIJANI

Share This
Klabu ya Chelsea sasa ina ruhusa ya kuendelea na mipango yake ya ukarabati na upanuzi wa uwanja wake wa Stamford Bridge ambao utagharimu zaidi ya bilioni 500 mara baada ya mipango hiyo kusimamishwa  hapo kabla kutokana na familia moja kulalamikia upanuzi huo.

Familia moja ambayo inaishi pembezoni kabisa mwa uwanja wa Stamford Bridge ambapo umbali wake kutoka kwenye mlango wa  nyumba hiyo inamoishi familia hiyo mpaka ulipo uwanja ni kama mita kadhaa ambazo ni karibu mpaka mtu akisimama na mpira uwanjani akipiga shuti basi unaifikia nyumba hiyo ilipo, familia hiyo iliomba kusimamishwa kwa ujenzi wa uwanja huo ambao umekuwa kwenye mipango ya muda mrefu ya kupanuliwa kutoka kubeba watu 40,000 mpaka watu 60,000 wakidai kama uwanja huo ukipanuliwa basi nyumba yao itakuwa imezibwa kabisa na ombi la familia hiyo likasikilizwa na serikali ya mtaa wa Fulham na kuutaka uongozi wa Chelsea ukae chini na familia hiyo iliyoishi hapo kwa miaka mingi ili kukubaliana nao.

Na ripoti zilizopo zinadai kuwa uongozi wa Chelsea ulikaa chini na familia hiyo na kuzungumza mpaka kuelewana na kupewa ruhusa ya kuendelea na ujenzi.

Kama Chelsea itaanza ujenzi huo basi utaifanya Chelsea isiutumie uwanja huo mpaka mwishoni mwa msimu wa 2019-2020 au wakaanza msimu wa 2021-2022 wakiwa uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment