KOCHA AELEZA SABABU YA KUACHANA NA CAHILL - Darajani 1905

KOCHA AELEZA SABABU YA KUACHANA NA CAHILL

Share This
Nahodha wa Chelsea, Gary Cahill ambaye ni raia wa Uingereza ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza ambacho kitacheza michezo ya kirafiki kujiandaa na michuano ya kombe la dunia itakayoanza mwezi Juni.

Kikosi hicho kinaongozwa na kocha Gareth Southgate kimeachana na nahodha huyo wa Chelsea huku pia kikikosa mchezaji yoyote kutokea klabuni hapo, kocha huyo alipoulizwa juu ya kukosekana kwa nyota huyo, alisema "Ilikuwa ni uamuzi mgumu sana kuufanya. Gary amecheza michezo mingi ya kufudhu, lakini pia ni mtu muhimu"

"Lakini tumewaita wachezaji ambao tutawaangalia ili kuwatumia kwa sasa na baada ya kipindi cha kiangazi" alisema kocha huyo.

GaryCahill amekuwa akitumika kwenye kikosi cha Uingereza toka mwaka 2010 huku akiichezea michezo 58 na kuifungia magoli 4.

No comments:

Post a Comment