Kocha wa Chelsea, Antonio Conte jana aliwashangaza wengi na kuibua mjadala mkubwa mara baada ya kuonekana kufurahi pamoja na nyota wa Barcelona, Lionel Messi ambaye alifunga magoli mawili katika ushindi wa klabu hiyo kuitupa nje ya mashindano klau ya Chelsea.
Mara baada ya mchezo kuisha, kocha huyo alionekana kuwa karibu na mshambuliaji huyo huku wakionekana wakiteta jambo, kocha huyo alipoulizwa ni nini alimwambia nyota huyo, Conte alijibu akisema "Unapopata nafasi ya kutoa pongezi kwa mchezaji, bora bora bora zaidi . Hii ni simulizi nzuri na kubwa kwa Mssi na Barcelona. Wachezaji kama hawa wanazaliwa mara moja ndani ya miaka 50. Tunamuongelea mchezaji mwenye ubora, uwezo na ufundi kisoka"
"Ni mchezaji bora sana. Tunamuongelea mchezaji anayeweza kuisaidia timu katika kila aina ya tukio la mwisho" alisema kocha huyo
CONTE AELEZA ALICHOMWAMBIA Messi MARA BAADA YA MCHEZO WA JANA
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment