Inaelezwa walinzi wa uwanja huo na mapolisi walianza kuwapiga mashabiki wa Chelsea waliokuwa wakitoka uwanjani na kujiandaa na safari ili kuondoka uwanjani hapo. Kuna video imesambaa ikiwaonyesha mashabiki hao wakipigwa na mapolisi hao wakati wakiwa wanatoka uwanjani jambo ambalo halikuwa sawa.
Klabu ya Chelsea imetoa taarifa kwamba kama kuna shabiki yoyote wa Chelsea alikuwa mmoja wa wahanga wa tukio hilo, basi awasilishe ushahidi wake iwe wa video au picha na kisha kama ukipatikana ushahidi huo basi itume malalamiko kwa chama cha soka barani Ulaya, UEFA.
Moja ya mashabiki hao alisema "Tukio hili lilitokea wakati tukiwa tunatoka uwanjani. Walinzi walitusukuma na kupita katikati yetu kinguvu, shabiki mmoja mdogo alibaki akiwa analia. Haikuwa sawa kabisa" alisema shabiki huyo.
Poleni mashabiki wenzetu, tunaamini hili litafanyiwa kazi ipasavyo...

No comments:
Post a Comment