Chelsea yaondoka na ushindi wa pili mnono - Darajani 1905

Chelsea yaondoka na ushindi wa pili mnono

Share This
Jioni ya leo kumechezeka mchezo mmoja ukiihusisha klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea FC Women ambao walikuwa ugenini kucheza mchezo wa Kombe la ligi maarufu kama Continental League Cup wakicheza dhidi ya klabu ya wanawake ya Crystal Palace.

Chelsea imefanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 0-4 katika mchezo huo na kuifanya kupata ushindi wake wa tatu katika michuano hiyo, lakini pia ukiwa ni ushindi wa pili mfululizo mara baada ya katikati ya wiki kupata ushindi wa magoli 0-5 dhidi ya Sarajevo katika michuano ya Klabu bingwa kwa wanawake barani Ulaya (UWL).

Magoli ya Bethany England ambaye amefunga mara mbili pamoja na jengine kutoka kwa Adelina Engman na jengine kutoka kwa Drew Spence yanaifanya klabu hiyo kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata mafanikio kwa msimu huu

Katika mchezo wa leo kikosi kilibadilika kidogo ukilimganisha na mchezo uliopita dhidi ya Sarajevo ambapo leo ilikuwa siku ya kwanza kwa mlinda mlango mpya, Lizzie Durrack kupata nafasi ya kuichezea Chelsea mchezo wa kwanza toka amesajiliwa katika dirisha kubwa la usajili. Nyota wengine kama Fran Kirby, Ji So-Yun, Ramona Bachmann na Millie Bright wote walianza wakiwa benchi.

➡Mchezo unaofafa
Bristol city Women vs Chelsea FC Women
Siku: Tarehe 19-Septemba
Michuano: Ligi kuu Uingereza kwa wanawake (FA WSL)

No comments:

Post a Comment