Eden Hazard ni tatizo kwa Chelsea - Darajani 1905

Eden Hazard ni tatizo kwa Chelsea

Share This
Eden Hazard alikuwa nyota wa mchezo katika mchezo uliopita wakati Chelsea ilipoibamiza Cardiff city magoli 4-1 uku Hazard akifunga magoli matatu na kufanikiwa kuingia katika orodha ya wachezaji 10 ambao wana magoli mengi kwa kipindi chote klabuni Chelsea, akishika nafasi ya tisa uku akiwa na magoli 94 toka aliposajiliwa mwaka 2012.

Lakini pia magoli hayo matatu yakimfanya kuwa mfungaji kinara katika orodha ya wafungaji katika ligi kuu Uingereza msimu huu wa 2018-2019 akiwa jumla ya magoli matano.
Nyota huyo mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo mitano ya ligi kuu na kufanikiwa kufunga magoli matano na kutoa pasi mbili za magoli.
Lakini mchambuzi wa soka ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool, John Barnes anaamini Hazard atakuja kuigharimu Chelsea endapo akipata majeraha.

"Litakuwa tatizo kwa Chelsea na kwa kocha Maurizio Sarri endapo ikitokea Hazard akapata majeraha. Amekuwa muhimili mkubwa katika ushambuliaji na kama ikitokea akipata majeraha litakuwa tatizo kubwa sana" amesema mchambuzi huyo.

Kocha Maurizio Sarri alipoulizwa kuhusu uwezo wa nyota huyo mara baada ya mchezo wa Chelsea dhidi ya Cardiff city kumalizika, alisema "Mwanzoni nilipofika hapa (Chelsea) nilifikiri Hazard ni moja kati ya wachezaji bora duniani. Lakini sasa naamini ni mchezaji bora duniani"

Hazard atakuwa sehemu ya kikosi kitakachomenyana dhidi ya PAOK katika mchezo wa ligi ya Ulaya (Europa League) siku ya alhamisi, mchezo utakaochezwa huko nchini Ugiriki.

No comments:

Post a Comment