Kepa atoa neno kuhusu nafasi yake Hispania - Darajani 1905

Kepa atoa neno kuhusu nafasi yake Hispania

Share This

Kumekuwa na taarifa ambazo bado sio kamili lakini zinasema mlinda mlango wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga anaweza kutumika kama mlinda mlango nambari moja katika timu ya taifa ya Hispania, wakati timu hiyo itakaposhuka uwanjani kucheza dhidi ya Bosnia & Herzegovina hapo kesho jumapili.

Taarifa hizi zimeibuka mara baada ya mlinda mlango nambari moja kwenye timu hiyo, David De Gea kuwa sehemu ya kipigo ambacho Hispania imekipata mbele ya Croatia kwa magoli 3-2.

Taarifa hizo zimemfanya Kepa atoe majibu alipoulizwa kuhusu nafasi hiyo ambapo alisema "Kwangu nitaendelea kufanya mazoezi kwa bidii na juhudi kubwa. Kila mtu anatamani kupata nafasi ya kucheza. Kama kocha akiona mtu anayefaa basi huyo ndiye atapewa nafasi."

Katika ngazi ya klabu kwenye ligi kuu Uingereza, Kepa amecheza michezo 12 uku akifungwa magoli 8 na kumaliza mchezo bila kufungwa katika michezo 6 wakati kwa upande wa De Gea ambaye ni mlinda mlango wa Man utd, amecheza michezo 12 uku akifungwa magoli 21 na kumaliza mchezo bila kufungwa katika mchezo mmoja tu.

No comments:

Post a Comment