Mwamuzi alifanya makosa Chelsea ilipotoa sare ya 4-4 dhidi ya Ajax - Darajani 1905

Mwamuzi alifanya makosa Chelsea ilipotoa sare ya 4-4 dhidi ya Ajax

Share This

Hiyo ni kwa mujibu wa gazeti la Telegraaf la nchini Uholanzi ambapo lilifanya makala na mwamuzi mmoja wakiujadili mchezo wa Chelsea dhidi ya mabingwa wa ligi kuu nchini kwao Uholanzi, Ajax kwenye mchezo ulioisha kwa sare ya 4-4 kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Klabu bingwa barani Ulaya, mchezo uliochezwa jijini London nchini Uingereza.

Mnamo dakika ya 70' ya mchezo huo matokeo yakiwa Chelsea 2-4 Ajax, mchezo ulisimama kwa muda na mwamuzi wa mchezo akatoa kadi nyekundu mbili akitoa kadi ya njano ya pili kwa Daley Blind ambaye alipewa kadi hiyo mara baada ya kuwachezea vibaya winga Christian Pulisic na mshambuliaji Tammy Abraham kisha wakati mwamuzi akiacha shambulizi liendelee, Joel Veltman akashika mpira ndani ya boksi la timu yake na kuzuia shuti la Callum Hudson-Odoi na mwamuzi kumpa kadi ya pili ya njano na  kuwafanya nyota wawili wa Ajax kutolewa kwa kadi nyekundu.


Gazeti hilo likiwa na mwamuzi mmoja anayetambulika likaandika kwamba mwamuzi wa mchezo huo hakuwa sawa kutoa kadi ya njano na  nyekundu kwa Veltman bila kuhakikisha maamuzi yake kupitia teknolojia ya VAR maana alifanya maamuzi kimakosa yaliyoigharimu Ajax kucheza wakiwa pungufu.


Kwa mujibu wa gazeti hilo linadai maamuzi ya mwamuzi wa  mchezo huo yalikuwa sababu kubwa kwa klabu hiyo kushindwa kufuzu kucheza hatua inayotafata ya 16 bora ambapo kwenye kundi zilifuzu Chelsea na Valencia ambao wao walifuzu mara baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa mwisho walipomenyana dhidi ya Ajax na kuwafunga bao 1-0.

No comments:

Post a Comment