Nyota huyo mwenye miaka 16 amekamilisha usajili huo unaotajwa kuwa na thamani ya euro 46,000 (Tsh. milioni 116).
Nyota huyo kinda anayecheza nafasi ya winga haswa winga wa kushoto anatajwa kuwa Ronaldo mpya wa Sweden na mara kadhaa amekuwa akihusishwa kutakiwa na klabu vigogo ikiwemo klabu ya Man utd ambayo mwaka 2018 ilimfanyia majaribio klabuni kwao.
Kocha wa timu ya akademi ya IFK, Jonas Olsson alipohojiwa na tovuti ya klabu yao alisema "Tunapenda kumtakia heri ya mafanikio kwa Edwin, japo tulitamani tuendelee kubaki nae lakini amekamilisha uhamisho wake kwenda Chelsea. Tunajivunia kuona tunazalisha wachezaji bora."
Andersson atajiunga na kikosi cha vijana cha Chelsea.
No comments:
Post a Comment