Zimesalia siku kadhaa kabla ya kuanza michuano ya kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2018 ambapo safari hii itatimua vumbi huko nchini Urusi kuanzia mwezi Juni.
Kuelekea kwenye michuano hiyo kumekua kukifanyika uteuzi wa wachezaji mbalimbali watakaoungana kwenye timu zao za taifa ili kushiriki michuano hiyo.
Timu kadhaa zishatangaza wachezaji wake 23 watakaoshiriki michuano hiyo ambapo kwa upande wa timu ya taifa ya Uingereza imewajumuisha wachezaji wawili kutoka Chelsea.
Nahodha wa Chelsea, Gary Cahill pamoja na Ruben Loftus-Cheek wote wamejumuishwa kwenye orodha hiyo ya wachezaji 23 watakaoshiriki michuano hiyo ya kombe la dunia mwaka huu.
No comments:
Post a Comment