Chama cha soka nchini Uingereza (FA) kimeitia hatiani klabu ya Chelsea kutokana na tukio lililotokea kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza wiki iliyopita wakati Chelsea ilipotoka suluhu ya 1-1 na klabu ya Huddersfield.
Klabu ya Chelsea inahukumiwa kwa kushindwa kuwazuia wachezaji wake ambao walimzonga mwamuzi wa mchezo huo Lee Mason wakimlalamikia juu ya kuamuru mpira uwe mapumziko badala ya kuiruhusu Chelsea ipige kona ambayo tayari ilishaandaliwa na Cesc Fabregas.
Mwamuzi huyo aliamuru mchezo kuisha kwa kipindi cha mapumziko wakati ambao Chelsea walikuwa wakijiandaa kupiga kona jambo ambalo liliwakera wachezaji wa Chelsea na kuanza kumzonga mwakuzi huyo. Wakati huo matokeo yalikua 1-1.
Mara baada ya tukio hilo, chama hicho cha soka kimeihukumu Chelsea kwa kuitoza paundi 20,000 kwa kushindwa kuwazuia wachezaji wake.
No comments:
Post a Comment