Wakala wa nyota wa Chelsea, Jorginho ameweka wazi uwezekano wa nyota huyo kuondoka klabuni hapo na kujiunga na kocha wa zamani wa Napoli na Chelsea, Maurizio Sarri ambaye alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Jorginho klabuni humo.
Akihojiwa na moja kati ya vyombo vya habari wakala huyo alipoulizwa kuhusu uwezekano wa nyota huyo kuondoka alisema "Ana maendeleo mazuri ndani ya Chelsea, lakini nina hakika zitatokea ofa nyingi kumtaka kwasababu kwa nafasi yake anayocheza hakuna mchezaji mwenye uwezo mkubwa anayetimiza majukumu kama yake."
Alipoulizwa kama Juventus inaweza kumnasa mteja wake, wakala huyo alisema "Kwanini isiwezekane? Naamini kabisa zitakuja klabu na ofa nzuri sana, inachotakiwa ni kukaa chini na Chelsea ili kuona tunafanyaje."
No comments:
Post a Comment