Nyota wa Chelsea, Mateo Kovacic ambaye ndani ya misimu minne amekuwa chini ya makocha watatu ambao ni Zinedine Zidane akiwa klabuni Real Madrid na baadae kusajiliwa kwa mkopo na kujiunga na Maurizio Sarri klabuni Chelsea na baadae kocha Frank Lampard wa Chelsea akakilisha uhamisho wake wa jumla.
Mateo Kovacic ameeleza tofauti iliyopo kwa makocha hao lakini pia akielezea na msimu wake ndani ya Chelsea;
"Naamini ana mwendelezo mzuri na mipango mikubwa, kama akipewa muda wa kutosha naamini anaweza kuleta mafanikio mengi makubwa."
"Msimu huu umekuwa msimu bora kwangu, ata kwa takwimu nimekuwa bora, nimefunga na kutoa pasi za mwisho. Nafikiri ni kwasababu nimeshayazoea mazingira ya Chelsea na jiji la London."
"Najisikia vizuri kucheza Chelsea na nimekuwa na msimu mzuri. Nafikiri hiki ndicho kipindi nilichocheza kwa ubora sana kwenye maisha yangu ya soka. Kwasababu nimekuwa nikiguaa mpira mara nyingi na nikikokota zaidi. Umekuwa ni msimu bora kwangu."
"Tofauti na msimu uliopita, nilikuwa nachezeshwa sehemu moja na kutopewa uhuru hivyo ikawa rahisi kutabirika, na wapinzani walitusoma, ilikuwa ngumu kwangu kuwa bora."
"Sarri alikuwa hataki tupige pasi ndefu kuanzia kwa mabeki kama timu pinzani haiji kutukaba, ikawa inatupa wakati mgumu muda mwengine, lakini kwa Lampard amekuwa akitupa uhuru na kutuagiza tucheze kutokana na tunavyoona mchezo unavyoenda."
"Zidane alikuwa bora pia, falsafa zake hazitofautiani sana na Lampard, wote wamenipatia ingawa Zidane ilitakiwa anipe nafasi zaidi kwenye klabu bingwa Ulaya."
"Chelsea ilipomtangaza kocha Lampard kama kocha mpya, sikuwa najua kipi nakitegemea kutoka kwake, lakini acha niwe mkweli na nikiri kwamba Lampard ni kocha wa kipekee sana."
"Lampard ameweza kuutumia ule uwezo wake na jina alilolitengeneza akiwa mchezaji kujitolea mfano mwenyewe na mara nyingine kuhusika kwa vitendo kuonyesha nini anataka, tofauti na Maurizio Sarri."
No comments:
Post a Comment