Kwa taarifa za chini chini, zinazoripotiwa na vyanzo kadhaa zinadai klabuni Chelsea kuna mzozo mkubwa unaoendelea kati ya kocha Frank Lampard na mkuu wa bodi ya Chelsea, Marina Granovskaia anayetimiza pia majukumu ya mkurugenzi wa michezo.
Taarifa hizo zinadai kwamba Frank Lamard haridhishwi na ubora wa kipa huyo raia wa Hispania mwenye miaka 25 na anataka nyota huyo auzwe kwenye dirisha kubwa lijalo wakati Marina Granovskaia ambaye alikamilisha uhamisho wa kipa huyo kutoka Athletico Club akitaka kipa huyo aendelee kupewa nafasi.
No comments:
Post a Comment