Ufafanuzi: Likizo ya Ligi kuu Uingereza - Darajani 1905

Ufafanuzi: Likizo ya Ligi kuu Uingereza

Share This

Kama umefatilia vyema ratiba ya ligi kuu Uingereza umeona mara baada ya Chelsea kucheza mchezo wake dhidi ya Leicester tarehe 1-Februari, mchezo mwengine unaofata itacheza dhidi ya Man utd tarehe 17-Februari.

Ushajiuliza kwanini siku ni nyingi sana kutoka  tarehe 1 mpaka tarehe 17?

Ufafanuzi upo hivi!
Muda huo umetengwa maalumu na bodi ya ligi kuu Uingereza, wakiipa jina la kipindi cha likizo cha kipindi cha baridi (winter break) ambapo hapo mwanzo hakikuwepo.

Kimetambulishwa kwa mara ya kwanza msimu huu kikiwa na lengo la kuzipa nafasi timu kupumzika na kujiweka sawa  mara baada  ya kipindi cha baridi ambapo hapo kabla ligi nyengine tofauti na ligi kuu ya Uingereza zilikuwa na likizo hii.

Kwa Uingereza ni ligi kuu tu ndiyo yenye likizo hii lakini kwa ligi za chini zitaendeleza michezo yake kama kawaida na hii yote ni kutokana na ligi hizo kuwa na ratiba ngumu haswa kutokana na ligi kuwa na  timu nyingi zaidi kuliko ligi kuu Uingereza.

Likizo hii inatajwa itabadilisha ratiba ya michezo ya Kombe la FA kutoka siku za mwisho wa wiki mpaka kuchezeka katikati ya wiki na kama mchezo ukiisha kwa sare basi zitaongezwa dakika 30 za nyongeza na mwisho wa siku mpaka penati sio kama ilivyozoeleka kwamba timu zikitoka sare mchezo wa kwanza zinarudiana kwenye uwanja wa timu iliyokuwa ugenini.

Timu za ligi kuu Uingereza zimechagua kutumia kipindi hiki kutimiza ratiba tofauti tofauti na zinavyoona sawa lakini Chelsea imeona iwape likizo wachezaji wake kwenda mapumzikoni na familia zao na ndiyo maana ukiwafatilia wachezaji kadhaa utaona wamejumuika sehemu mbalimbali na familia zao.

No comments:

Post a Comment