Timo Werner aelezea mipango yake juu ya mustakabali wake - Darajani 1905

Timo Werner aelezea mipango yake juu ya mustakabali wake

Share This
Dirisha dogo la usajili la mwezi januari limepita uku Chelsea ikiwa haijasajili mchezaji yeyote licha ya hapo kushinda rufaa yake ya kufunguliwa kifungo cha kutosajili kwa madirisha mawili.



Moja kati ya wachezaji ambao wamehusishwa kwa karibu kutakiwa na Chelsea ni mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Ujerumani, Timo Werner ambapo usajili wake ulishindikana kutimia.

Nyota huyo amehojiwa na moja kati ya magazeti ya michezo barani Ulaya kuhusu mustakabali wake na mipango yake kwenye soka lake.

"Bado tuna ratiba muhimu ambayo tunatakiwa kuikamilisha kwa msimu huu. Hivyo sikuona haja ya kuondoka kwenye dirisha hili lililopita."

"Lakini pia hakuna mchezaji asiyetaka kujiunga na timu yenye mipango na mbio za kuwania ubingwa wa Ulaya, hivyo siwezi kubisha kwamba natamani kucheza klabu yenye hadhi hiyo."

"Najiona siku moja nikiwa mchezaji wa timu kutoka nje ya Ujerumani, lakini mpaka sasa sijajua ni timu gani nitakuja kuichezea." amesema nyota huyo raia wa Ujerumani.

Moja kati ya sababu inayotajwa chini kwa chini kuhusu nyota huyo kuamua kusalia Bundesliga kwa dirisha hili ni kwamba hakutaka kuondoka kwenda timu nyengine ambapo anaweza kupambana tena kuwa kwenye fomu kama aliyonayo kwasasa Leipzig hivyo inaweza kumfanya akose nafasi kwenye timu yake ya taifa itakayoshiriki michuano ya Euro mwaka huu wa 2020.

No comments:

Post a Comment