Pulisic kurejea siku ya kivumbi dhidi ya Man utd - Darajani 1905

Pulisic kurejea siku ya kivumbi dhidi ya Man utd

Share This
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, nyota wa Chelsea raia wa Marekani, Christian Pulisic anategemewa kurejea uwanjani siku ya kivumbi cha Chelsea dhidi ya Man utd tarehe 17-Februari.

Nyota huyo amekuwa nje toka siku ya mwisho alipoitumikia Chelsea kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Brighton siku ya tarehe 1-Januari mwaka huu na inategemewa atarejea uwanjani siku hiyo ambapo Chelsea itakuwa uwanjani kucheza mchezo wake wa 26 wa ligi kuu Uingereza.

Kwasasa nyota huyo anaonekana yupo imara na tayari ameshaanza mazoezi uku kocha Frank Lampard akisema mapumziko haya ya kipindi cha baridi yamekuja wakati sahihi ambapo yatawapa nafasi nyota wake kupata mapumziko na kujiweka sawa, wakiwemo Christian Pulisic na Ruben Loftus-Cheek, nyota ambao wanatazamiwa kurejea siku ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment