Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star limeripoti kwamba kocha Frank Lampard haridhishwi na kiwango na uwezo wa kipa nambari moja klabuni hapo, Kepa Arrizabalaga.
Hivyo kuna taarifa kwamba kocha huyo ameingia sokoni kumnasa kipa atakayeziba pengo la mlinda mlango huyo mwenye miaka 25 kutoka nchini Hispania.
Kipa Nick Pope wa Burnley ambaye ni raia wa Uingereza anatajwa kuwepo kwenye kinyang'anyiro hicho cha kuwaniwa na klabu hiyo ambayo inategemewa kuwa na mabadiliko makubwa kwenye dirisha kubwa la usajili lijalo.
No comments:
Post a Comment