Kumbe hii ndiyo sababu iliyomfanya Florent Malouda aondoke Chelsea - Darajani 1905

Kumbe hii ndiyo sababu iliyomfanya Florent Malouda aondoke Chelsea

Share This
Ni nini unakikumbuka msimu wa 2012-2013 kilichomtokea Florent Malouda? unakumbuka aliondoka vizuri Chelsea?
Kwa wale wafatiliaji wazuri watakumbuka msimu wa mwisho wa winga huyo klabuni Chelsea ulikuwa na matatizo mengi yaliyojaa migogoro akikorofishana na uongozi wa Chelsea ambao ulikasirishwa na kitendo cha mfaransa huyo kukataa kuondoka Chelsea licha ya klabu kadhaa kuhitaji huduma yake uku sababu iliyomfanya kukataa kuondoka ni klabu zilizomtaka kutaka kumpunguzia mshahara wa paundi 80,000 kwa wiki aliokuwa analipwa Chelsea.
Mara baada ya kukataa kupunguziwa mshahara kutoka klabu zilizomtaka, uongozi wa Chelsea ukamuadhibu kwa kuamuru benchi la ufundi kutomjumuisha kwenye kikosi chochote ambacho Chelsea ilishuka uwanjani kwa msimu wa 2012-2013, lakini pia akakataliwa kuhudhuria mazoezi ya Chelsea ya wakubwa na badala yake akawa anafanya mazoezi na kikosi cha vijana tu.
Nyota huyo ambaye kwasasa anacheza soka nchini Luxembourg akiwa ana miaka 38 alipohojiwa kuhusu sakata hilo alisema, "Kiukweli kwa mafanikio niliyoyafikia nikiwa Chelsea sidhani kama ilikuwa sahihi kunifanyia vile walivyonifanyia."

"Mashabiki wananipenda sana na mara zote wamekuwa pamoja namimi lakini tatizo lipo kwenye uongozi wa klabu. Nilifanya mengi makubwa sikustahili kulipwa kwa yale niliyofanyiwa."

"Niliamua kukaa kimya na kuwaacha wanifanyie vile walivyotaka ingawa sikupendezwa nayo." alisema nyota huyo ambaye aliichezea Chelsea michezo 228 uku akiifungia magoli 45 na kutengeneza mengine 43 kwa kutoa pasi za mwisho.
Lakini pia alishinda mataji ya Klabu bingwa Ulaya msimu wa 2012-2013, Ligi kuu Uingereza msimu wa 2009-2010, Kombe la FA mara tatu na Ngao ya Hisani mara moja.


Nyota huyo aliondoka Chelsea akiwa kama mchezaji huru na akajiunga na klabu ya Trabzonspor.

No comments:

Post a Comment