Mchezo huo ulioisha kwa Trabzonspor kushinda 2-1 ukiwa ni mchezo wenye upinzani mkubwa ndani ya uwanja na nje ya uwanja, nyota huyo raia wa Nigeria alipata dhahma ya kubaguliwa rangi na mashabiki wa timu pinzani na klabu yake ya Trabzonspor imethibisha kwamba kesi hiyo imepelekwa kwenye vyombo vya sheria kuwashtaki mashabiki wa timu pinzani.
Inaelezwa kwamba Obi Mikel amekuwa akipokea jumbe za ubaguzi wa rangi na kusemwa vibaya lakini pia kundi la mashabiki wachache wakimfata na kumbagua waziwazi.
Nyota huyo mwenye miaka 32 anadai pia ubaguzi huo umewakumba pia familia yake ambayo inamjumuisha mke mmoja na watoto wawili wakike.
No comments:
Post a Comment