RLC arejea uwanjani, leo ameshuka dimbani - Darajani 1905

RLC arejea uwanjani, leo ameshuka dimbani

Share This
Wakati nyota wenzake wa kikosi cha wakubwa wakiwa mapumzikoni kwenye likizo ya majira ya baridi ya ligi kuu Uingereza, nyota wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek leo alikuwa uwanjani akicheza mchezo wa kirafiki kabla ya kurejea kwenye kikosi cha wakubwa.


Mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye viwanja vya mazoezi vya Cobham ilimpa nafasi Loftus-Cheek kucheza mechi ya kujiweka sawa na kuwaongoza kikosi cha vijana cha Chelsea kucheza dhidi ya Brentford B kwenye mchezo wa kufungwa geti (mashabiki hawakuruhusiwa kuingia) ambapo uliisha kwa Chelsea kupoteza 2-0.

Loftus-Cheek alicheza kwa dakika 60, zikiwa ni dakika zake za kwanza uwanjani toka alipoumia miezi tisa iliyopita.

Billy Gilmour pia alikuwa sehemu ya mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment