Chelsea yaorodhesha kikosi kitakachocheza Uefa, yamjumuisha kipa kinda - Darajani 1905

Chelsea yaorodhesha kikosi kitakachocheza Uefa, yamjumuisha kipa kinda

Share This
Chelsea imemjumuisha kinda kinda kwenye kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya Uefa.


Kipa kinda mwenye miaka 18 raia wa Ivory Coast, Nicolas Tie amejumuishwa kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza michuano hiyo kwenye kikosi cha kundi B.

Amejumuishwa kwenye kikosi hicho akiwa ni moja kati ya wachezaji watakaoziba pengo la nyota Marc Guehi na George McEachran ambao wametolewa kwa mkopo kwenda Swansea na SC Cambuur.


Kikosi cha kundi B ndicho kikosi gani?
Kikosi cha kundi B ni kikosi cha wachezaji kinachojumuisha wachezaji kutoka timu za vijana za akademi kwa timu husika.

Kwa kawaida huwa kuna makundi mawili, kundi la kwanza ni kundi A ambalo linakuwa na wachezaji 25 wakiwemo makipa wawili na hiki kinajumuisha kikosi cha kwanza cha timu ya wakubwa.

Na kundi B ni kikosi kinachowajumuisha wachezaji wa akademi iwe bado wanacheza kwenye akademi ama walizalishwa na akademi hapo kabla ambao hawa wanaweza kutumika na timu kwenye michuano hiyo ya klabu bingwa Ulaya bila ata kuwepo kwenye orodha ile ya wachezaji 25.

Kikosi kitakachocheza michuano hiyo;

Makipa: Kepa Arrizabalaga, Willy Caballero, Jamie Cumming*, Nicolas Tie*

Mabeki: Cesar Azpilicueta, Marcos Alonso, Emerson Palmieri, Antonio Rudiger, Andreas Christensen, Kurt Zouma, Fikayo Tomori, Reece James*

Viungo: Jorginho, N'Golo Kante, Mateo Kovacic, Ross Barkley, Ruben Loftus-Cheek, Billy Gilmour*, Mason Mount*

Washambuliaji: Willian, Pedro, Tammy Abraham, Christian Pulisic, Olivier Giroud, Michy Batshuayi, Callum Hudson-Odoi*

Ufunguo:

Wachezaji wenye nyota (*) ndiyo waliowekwa kwenye orodha B

No comments:

Post a Comment