UCHAMBUZI; Je, Hazard atabaki Chelsea? - Darajani 1905

UCHAMBUZI; Je, Hazard atabaki Chelsea?

Share This

Leo nataka nifanye uchambuzi kuhusu Eden Hazard, haswa kuhusu mustakabali wake kama atabaki klabuni Chelsea au atatimkia Real Madrid kama tetesi zinavyosema.

Lakini uchambuzi wangu nataka niufanye kwa kupitia kauli zake mwenyewe ambazo mara kadhaa amekuwa akiziongea.

Kauli ya kwanza aliwai kusema "Nitabeba Kombe la Dunia nikiwa Ubelgiji na kushinda tuzo ya uchezaji bora nikiwa Chelsea." kauli hii aliitoa wakati alipoulizwa kuhusu nafasi yake ya kushinda tuzo ya uchezaji bora.

Kauli hiyo ukiitafsiri ni kama alimaanisha haitaji kuondoka Chelsea ili ashinde uchezaji bora yaani kwa maana nyengine unaweza kusema ataendelea kubaki Chelsea kwa muda mrefu.

Kauli ya pili aliwai kusema "Kucheza Real Madrid imekuwa ndoto yangu ya muda mrefu, lakini sitorazimisha kuondoka Chelsea...", kauli hii inamaanisha kwamba kuondoka Chelsea hatolazimisha lakini anatamani kuondoka Chelsea.

Kauli ya tatu nataka turudi nyuma kidogo, kabla Thibaut Courtois hajaondoka alisema "Atakaloliamua Courtois basi nami nitafanya hivyohivyo." kauli hii inamaanisha kama Courtois (ambaye ni mbelgiji mwenzake) akiamua kuondoka Chelsea basi naye ataondoka na kama akibaki basi naye atabaki. Ingawa amesema hatolazimisha kuondoka Chelsea lakini kauli hii nahisi bado haijafa.

Kauli ya nne ni kuhusu kusema kwake kitakachotokea baadae tusubiri msimu uishe. Hii kauli ndiyo inayozidi kuniumiza kichwa.

Ukweli ni kwamba ukweli wa kubaki kwake Chelsea anaujua mwenyewe labda na familia yake tu. Ukizifatilia vizuri kauli hizi unaona kuna uwezekano mkubwa akaondoka japo amesema hatolazimisha.

Mkataba wake unamalizika mwaka 2020, na endapo msimu huu ukimalizika bila kusaini mkataba mpya na msimu ujao wa 2019-2020 ukianza basi Chelsea itaingia kwenye kizungumkuti mkubwa.

Kama atakuwa bado hajasaini mkataba mpya, basi italazimika kumuuza tena kwa dau dogo kabla ya mkataba wake kumalizika na kuondoka bure.

Itakuwa amekamilisha alichokisema, hatolazimisha kuondoka lakini Chelsea italazimika kumuuza kwenda Real Madrid ambapo huko ndiko ndoto zake zilipo.

Kubwa ambalo Chelsea inatakiwa kulifanya kwasasa ni kuhakikisha inampa mkataba mpya kabla ya msimu ujao kuanza, itakuwa ni ngumu sana kumzuia.

No comments:

Post a Comment