Pulisic mlangoni kuingia Chelsea - Darajani 1905

Pulisic mlangoni kuingia Chelsea

Share This

Chelsea inaweza kukamilisha usajili wa kumnasa nyota wa klabu ya Borrusia Dortmund, Christian Pulisic.

Hiyo ni kutokana na taarifa iliyotolewa na gazeti moja nchini Uingereza ambalo limeeleza kwamba Dortmund walikuwa tayari kumuuza nyota huyo mwishoni mwa msimu huu katika dirisha kubwa la usajili lakini Chelsea inaweza kukamilisha usajili wake mwezi Januari katika dirisha dogo la usajili.

Hapo kabla dau la nyota huyo raia wa Marekani lililikuwa linatajwa kufikia paundi milioni 70 (Tsh. Bilioni 207) lakini dau hilo linaweza kupungua kutokana na Dortmund kuogopa nyota huyo kuweza kuondoka bure ambapo mkataba wake na klabu hiyo unaisha mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment