Kukiwa kumefikia katikati ya msimu kwa ligi kuu Uingereza huku Chelsea ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu Uingereza huku kwa upande wa ligi ya mabingwa Ulaya ikipangwa kumenyana na Barcelona katika hatua ya 16 bora, chombo cha habari cha ESPN ambacho kimekuwa kikijihusisha na michezo ikiwamo soka kimemtabiria kocha wa Chelsea, Antonio Conte atakavyomaliza msimu kuwa atafanikiwa kuifunga na kuitoa klabu ya Barcelona katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Barcelona imepangwa kucheza na Chelsea ambapo katika mchezo wa kwanza klabu hizo zitaanzia nyumbani kwa Chelsea, Stamford Bridge huku katika mchezo wa pili Chelsea ikisafiri na kuifata Barcelona katika uwanja wa Camp Nou.
Utabiri wa ESPN kwa Chelsea;
Ligi kuu Uingereza; Nafasi ya 3
Ligi ya mabingwa Ulaya; Robo-fainali
Carabao Cup; Nusu fainali
FA Cup; Mshindi
Ligi kuu Uingereza; Nafasi ya 3
Ligi ya mabingwa Ulaya; Robo-fainali
Carabao Cup; Nusu fainali
FA Cup; Mshindi
No comments:
Post a Comment