Rais wa klabu hiyo ya Exeter city, ndugu Julian Tagg amesema "tutawajulisha mashabiki kuhusu kitakachoendelea kwa Ethan, uhusiano wetu na Chelsea upo vizuri kwa maana hiyo tutakaa nao chini kuzungumza suala hili.
Ethan Ampadu alisajiliwa kutoka Exeter city katika dirisha kubwa la usajili la kipindi cha kiangazi bila ya Chelsea na Exeter kufanya makubaliano ya kiasi gani Chelsea itawagharimu ili kumpata nyota huyo. Na sasa Exeter ndio ipo kwenye mipango ya kukutana na bodi ya Chelsea ili kuzungumzia taarifa ya nyota huyoa laiyewai kutakiwa na Manyumbu (Man utd) pamoja na Arsenal.
No comments:
Post a Comment