Kiungo na nyota wa zamani wa Chelsea, Juan Mata ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Manyumbu(Man utd) hapo jana aliifungia klabu yake hiyo magoli mawili katika mchezo dhidi ya Leicester city katika uwanja wa King Power, mchezo ulioisha kwa suluhu ya 2-2.
Juan Mata baada ya kufunga goli la pili dakika ya 60 kwa njia ya mpira wa adhabu alishangilia kwa kuweka mikono kama anasali na kusema maana ya ushangiliaji huo ni kulitoa goli hilo kama zawadi kwa watoto wanaopatikana katika mpango Organization for Social Change Awareness and Responsibility (OSCAR) inayopatikana jijini Mumbai, India.
Taasisi hiyo ilimtembelea nyota huyo wa zamani wa Chelsea ambaye ni raia wa Hispania ambapo taasisi hiyo ilimtembelea mwezi oktoba.
Oscar ni taasisi iliyoanzishwa mwaka 2006 huko nchini India ikiwa katika jiji la Mumbai ikiwakusanya watoto na kuwapa elimu uku ikitumia soka au michezo kuwajumuisha kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment