Mshambuliaji na nyota wa klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa, Jean Michael Seri anatakiwa na Chelsea.
Seri ambaye kwa sasa ana miaka 27 akiwa ni raia wa Ivory Coast amekuwa akizitamanisha klabu kubwa barani Ulaya kutokana na uwezo wake mkubwa huku klabu kama Barcelona ikipeleka maombi ya kumsajili nyota huyo huku wakiwa na dau la paundi milioni 35 lakini likakataliwa.
Chelsea inamtaka nyota huyo anayetomea taifa alilowai kutokea gwiji wa Chelsea, Didier Drogba ambapo Conte ana mpango wa kukiimarisha kikosi huku akikabiliwa na michezo migumu kuanzia mwezi februari mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment