PL; FT, EVERTON 0-0 CHELSEA - Darajani 1905

PL; FT, EVERTON 0-0 CHELSEA

Share This
Hatimaye Everton inapata suluhu kwa mara ya kwanza toka mwaka 2015 dhidi ya Chelsea katika michuano ya ligi kuu Uingereza huku Chelsea ikiweka rekodi mpya kwa kucheza mchezo wake wa 5000 toka kuanzishwa kwake mwaka 1905.
Ulikuwa ni mchezo muhimu kwa Chelsea katika kujiweka katika nafasi nzuri ya kulitetea taji lake la ligi kuu ikiwa kama bingwa mtetezi.
Mchezo umeisha kwa suluhu huku Chelsea ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga ambapo imetengeneza nafasi 8 huku Everton wakishindwa kutengeneza nafasi hata moja huku wakimkosa mshambuliaji wao Wayne Rooney kutokana na majeruhi aliyoyapata.
Kwa matokeo haya, Chelsea inatimiza mchezo wake wa 19 huku ikiwa na alama 39 ikiachwa alama mbili na Manyumbu(Man utd) inayoshika nafasi ya tatu huku ikiachwa na Mama site (Man city) kwa alama 12 wakiwa kileleni.

No comments:

Post a Comment