PL; HT, EVERTON 0-0 CHELSEA, ANATAKIWA NAMBA 9 - Darajani 1905

PL; HT, EVERTON 0-0 CHELSEA, ANATAKIWA NAMBA 9

Share This

Mpira ni mapumziko katika dimba la Goodison Park, huku hali haijawa shwari bado ambapo hakuna timu iliyoliona lango la mwenzake.

Chelsea imetawala mchezo huku ikikosa nafasi kadhaa ambapo nyingi zingeweza kubadilishwa na kuwa magoli kama angepatikana mshambuliaji wa kati wa kiasili mara baada ya Alvaro Morata kufungiwa kucheza mchezo huu.

Eden Hazard ndiye anacheza kama mshambuliaji wa kati ingawa kiasili ni mshambuliaji anayetokea pembeni kuingia kati.

Pedro na Willian ni kama hawajawa sawa kwa mchezo huu lakini Antonio Conte anaweza akawaweka sawa na kuwafanya wawe katika hali yao ya kawaida.

Christensen bado anaendeleza ubora wake huku Bakayoko akiendelea kupevuka na kucheza vizuri zaidi, Antonio Rudiger yupo sawa wakati kwa Marcos Alonso naye akiwa kwenye ubora wake.

Huenda mabadiliko yatafanyika ambapo Fabregas anaweza akaingia ili kupenyeza pasi zake kuwatengenezea nafasi akina Hazard na wenzake ili walete furaha Darajani.

No comments:

Post a Comment