Ross Barkley jana alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa kama mchezaji wa Chelsea toka kusajiliwa kwa dau la paundi milioni 15 kutoka Everton, ingawa mchezo huo haukua maalumu maana ulipangwa kama mchezo wa kirafiki ili kukiangalia kiwango na uwezo wa nyota huyo mpya klabuni Chelsea.
Barkley alifunga mara mbili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya majirani wa Chelsea jijini London, QPR huku akitajwa kuonyesha kiwango kikubwa licha ya kutokea kwenye majeruhi yaliyomweka nje kwa miezi saba.
Mchezo huo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea maarufu kama Cobham stadium ambao haukushuhudiwa na shabiki yoyote uliandaliwa ili kuona maendeleo ya Barkley kutokana na kutoruhusiwa kucheza mchezo wa FA ambao Chelsea ilishinda kwa penati 5-3 dhidi ya Norwich kutokana na kuripotiwa kuwa usajili wa mchezaji huyo ulikamilika muda ambao wachezaji waliotakiwa kushiriki kombe ilo la FA kuwa tayari majina yao yashakaririshwa kwa uongozi wa chama cha soka Uingereza, FA.
Barkley anaweza akawepo katika mchezo wa jumamosi ambapo Chelsea itasafiri kuifata Brighton nyumbani kwao muda saa 9:30 jioni (Saa 15:30) katika mchezo wa ligi kuu.
No comments:
Post a Comment