CHELSEA HATIHATI KUMKOSA NYOTA WA UJERUMANI - Darajani 1905

CHELSEA HATIHATI KUMKOSA NYOTA WA UJERUMANI

Share This
Moja ya nyota ambao wanahusishwa kutakiwa na Chelsea katika dirisha hili la usajili ambao hawatajwi sana, yani Chelsea ni kama inataka kuwanasa kimyakimya bila kutoa taarifa ni mshambuliaji kinda raia wa Ujerumani anayeichezea klabu ya Hamburger ya nchini humo, Jann Fierte Arp ambaye kwa sasa ana miaka 18.

Chelsea inadaiwa kumfukuzia nyota huyo ila kuna taarifa ambazo sio nzuri juu ya usajili huo ambapo klabu hiyo ya Hamburger inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga imeandaa mazungumzo na nyota huyo ili kumshawishi asaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki klabuni hapo.

Nyota huyo amebakisha mwaka mmoja na miezi sita katika mkataba wake wa sasa ambao unaisha mwaka 2019 na analipwa euro 500,000 kwa mwaka na sasa klabu hiyo imepanga kumpa mkataba mpya utakaomweka klabuni hapo mpaka mwaka 2023 huku akiongezewa mshahara mpaka kufikia euro milioni 2.

Kinda huyo mpaka sasa ameichezea Hamburger michezo kumi na kifungia magoli mawili.

No comments:

Post a Comment