Chelsea inatajwa kufikia makubaliano na klabu ya Arsenyani (Arsenal) ili kumnasa nyota wa klabu hiyo, Olivier Giroud kwa dau linaloelezwa kufikia paundi milioni 18.
Chelsea imeanza kuhusishwa kumnasa nyota huyo raia wa Ufaransa katika siku mbili hizi huku mpango wa kumsajili Edin Dzeko ukionekana kufa mara baada ya kushindwa kuelewana na klabu yake ya As Roma.
Giroud alisajiliwa na Arsenyani akitokea klabu ya Montpellier ya nchini Ufaransa kwa dau la paundi milioni paundi milioni 9.6 msimu 2012/2013 na sasa anajiunga Chelsea akiwa ana miaka 31.
Darajani 1905 inaelewa usajili huu wa Giroud umefanywa na Chelsea kwa malengo ya muda mfupi na sio kumtumia kwa misimu ijayo na inaamini kigezo kilichotumika katika usajili wa kumsaka mshambuliaji katika dirisha hili sio umri wa mchezaji ila imetumia dirisha hili kumtafuta mshambuliaji mwenye uzoefu na anayeifahamu ligi kuu ndio maana imehusishwa na nyota kadhaa waliowai kucheza Uingereza kama Edin Dzeko na hata wale ambao bado wapo Uingereza kama Peter Crouch, Andy Carroll, Ashley Barnes na Islam Slimani ambao wote hawakutakiwa kwa malengo ya muda mrefu, ila ya muda mfupi kutokana na umri wao.
No comments:
Post a Comment