Klabu ya As Roma inaweza kupokea ofa muda wowote kuanzia sasa juu ya nyota wao, Emerson Palmeira ambaye anacheza nafasi ya mlinzi wa kushoto akitajwa kuwaniwa na Chelsea.
Chelsea inamtafuta nyota atakayeweza kupambania nafasi ya mlinzi wa kushoto ambapo upande huo unachezewa na Marcos Alonso ambaye anaonekana kutokupata upinzani.
Lakini Chelsea inamtaka nyota huyo ambaye kwa sasa ana miaka 23 lakini amekuwa na majeruhi toka mwaka jana mwezi Mei.
Kama Chelsea ikifanikiwa kumpata Emerson basi atakuwa nyota wa pili kuvutwa na Chelsea ikiwa chini ya Conte kutokea klabuni As Roma ambapo kabla alisajiliwa Antonio Rudiger.
No comments:
Post a Comment