Klabu ya Chelsea itapata tabu kumzuia nyota wake N'Golo Kante ambaye amefanywa kuwa chaguo la kwanza kwa klabu ya PSG inayotokea nchini kwao Ufaransa.
PSG inamtaka nyota huyo ili kujiweka sawa katika michuano inayoshiriki na huku ubora wa nyota huyo umeonyesha kuivutia klabu hiyo ya jiji la Paris.
Kante aliyeweka rekodi ya kufanikiwa kutwaa taji la ligi kuu mara mbili mfululizo akiwa na klabu mbili tofauti alipofanya hivyo alipokuwa klabuni Leicester na baadae kuisaidia Chelsea huku akitajwa kuwa sababu ya mafanikio kwa klabu hizo na huku akishinda tunzo kadhaa akiwa kama mchezaji bora wa msimu kwa ligi kuu Uingereza na hata kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwa mwaka 2017 nchini kwao Ufaransa
Kuna kazi ngumu kwa Chelsea kumzuia nyota huyo asiungane na PSG kutokana na klabu hiyo kukubali kuwa tayari kutumia fungu kubwa la pesa katika kumsajili nyota inayemtaka.
No comments:
Post a Comment