CONTE AWAJIBU MASHABIKI WA CHELSEA - Darajani 1905

CONTE AWAJIBU MASHABIKI WA CHELSEA

Share This

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amewajibu mashabiki waliojitokeza kwenye mchezo wa Chelsea ilipomenyana dhidi ya Leicester, jumamosi iliyopita huku mchezo huo wa ligi kuu ukiisha kwa sare ya 0-0.

Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kwenye mchezo huo walianza kuwazomea wachezaji wa Chelsea mara baada ya kutokuonyesha mchezo mzuri huku ikifululiza kucheza mchezo wa tatu bila kufunga goli.

"Najibu hilo swali la kuulizwa nilichukuliaje mashabiki walipokuwa wanazomea, muhimu ni kutumia asilimia 120 ya uwezo wako ingawa sisi tunajaribu kutumia zaidi ya hapo , muhimu ni kupambana kwa uwezo wako wote uwanjani kwa ajili ya timu iwe umefungwa au umeshinda muhimu ni kupambana na kujitoa kwa ajili ya timu" alisema kocha Antonio Conte.

Kutokana na matokeo ya jana ambapo klabu ya Liverpumba(Liverpool) kupata ushindi wa 4-3 dhidi ya Mama site(Man city), Chelsea imeshuka kwenye msimamo wa ligi kuu kutoka nafasi ya tatu mpaka nafasi ya nne ikiachwa na Liverpumba kwa tofauti ya magoli.

No comments:

Post a Comment