DZEKO NA EMERSON KUTUA CHELSEA MUDA WOWOTE - Darajani 1905

DZEKO NA EMERSON KUTUA CHELSEA MUDA WOWOTE

Share This

Nyota wa As Roma ambaye ni raia wa Bosnia, Edin Dzeko anaweza kutua Chelsea muda wowote kuanzia sasa mara baada ya kutoka taarifa kuwa Chelsea imeshakubaliana na klabu anayoichezea ya As Roma ili nyota huyo atue Darajani huku kilichobaki ni wakala wake kusafiri mpaka London ili afanye makubaliano binafsi juu ya nyota huyo kutua.

Taarifa zinadai Chelsea inakaribia kutoa paundi milioni 44 ili kumnasa nyota huyo pamoja na mlinzi wa kushoto wa klabuni hapo Emerson Palmeira ambaye wakala wake ameshafanya makubaliano na Chelsea na kilichokuwa kinasubiriwa ni klabu kumalizana.

Wakala wa Dzeko anaweza akasafiri leo jumatatu kuweza kutua London ili afanye makubaliano na Chelsea juu ya mahitaji binafsi ya nyota huyo huku usajili ukitajwa kukaribia kukamilika kesho jumanne ambapo wachezaji hao watatua London kukamilisha usajili.

No comments:

Post a Comment