Nyota wa zamani wa klabu ya Liverpumba (Liverpool) ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa michezo, Jamie Carragher amesema ingekuwa vyema kwa Arsenyani (Arsenal) ingemtumia kocha wa Chelsea, Antonio Conte kuwa mrithi wa Arsene Wenger klabuni kwao kama kocha huyo akiondoka.
"Sidhani kama kuna mbadala sahihi atakayeweza kuziba vyema pengo la Arsene Wenger kama Conte. Arsenal inamhitaji mtu wa kariba kama Conte. Utakuwa moja ya chaguzi sahihi katika historia ya ligi kuu." alisema mchambuzi huyo.
"Chelsea inatakiwa ikae vizuri na Conte, sio kwa kuwa tu ataipatia mafanikio Chelsea ila huenda wakimuachia atakuja kuwaadhibu atakapoenda kwa wapinzani"
"Kama bodi ya Chelsea haiwezi kuliona hilo, basi Arsenal inabidi wafanye wawezalo kuhakikisha jambo ilo linatokea" alisema Carragher.
Conte amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni Chelsea ingawa mwenyewe amekuwa akipinga kila akifanya mkutano na waandishi wa habari, na kumekuwa na baadhi ya makocha wamekuwa wakitajwa kuiwania nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment