CHELSEA YAHUSISHWA NA MSHAMBULIAJI MWENGINE - Darajani 1905

CHELSEA YAHUSISHWA NA MSHAMBULIAJI MWENGINE

Share This
Chelsea imehusishwa kumuwinda nyota wa klabu ya West Ham, Marko Arnautovic ili atue Darajani katika dirisha hili la usajili ili kuweza kutengeneza safu bora ya ushambuliaji. Nyota huyo anatajwa kuingia kwenye rada za Chelsea lakini akitajwa kuchukuliwa kama mpango wa kumsajili nyota wa As Roma, Edin Dzeko.

Arnautovic amejiunga na West Ham mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya Stoke city na anaweza akaachana na klabu hiyo katika dirisha hili la usajili  endapo tu mpango wa nyota Dzeko ukaenda kombo.

Chanzo kimoja kimeitaarifu Sky Sports kuwa Chelsea inamuwinda mshambuliaji huyo kutoka West Ham na anaweza kuingia kwenye orodha ya washambuliaji wanaowindwa huku ikiripotiwa kuwa kocha Antonio Conte anamtafuta mtu atakayeweza kusaidia mashambulizi huku Michy Batshuayi akitajwa kutolewa kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment