Habari zilizogaa kwenye mitandao mingi haswa chanzo kikuu kikiwa ni chombo cha habari cha nchini Italia kinadai kuwa nyota klabu ya nchini humo ya As Roma, Edin Dzeko anaweza akatangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Chelsea muda wowote kuanzia sasa kutokana na wakala wa nyota huyo anayeitwa Irfan Redzepagic amepanda ndege kusafiri mpaka Uingereza ili kukamilisha usajili wa nyota huyo ambaye mwezi Machi anatimiza miaka 32.
Wakala huyo anatajwa kufika Chelsea ili kumalizana juu ya mahitaji ya mchezaji huyo kukielezwa dau la paundi milioni 52 (Paundi milioni 44+Paundi milioni 8 kwa bonasi) ndicho kitakachoigharimu Chelsea ili kumpata nyota huyo pamoja na mlinzi wa klabu hiyo ya Roma, Emerson Palmieri.
Dzeko alibakiza miaka miwili kwenye mkataba wake klabuni As Roma na alikuwa akilipwa paundi 76,000 kwa wiki na mapaka anaondoka klabuni hapo kujiunga na Chelsea ameshaichezea michezo 117 na kuifungia magoli 61.
No comments:
Post a Comment