Nyota wa klabu ya Chelsea, Charly Musonda Jr ambaye ni raia wa Ubelgiji ingawa ana asili ya Afrika kwa upande wa baba yake ambaye ni raia wa Zambia huenda akajiunga na klabu moja wapo inayoshiriki ligi kuu Uingereza kwa mkopo ambapo kwa sasa kuna timu kadhaa zimeonyesha nia ya kumtaka nyota huyo.
Newcastle, West Brom na Afc Bournemouth ni baadhi ya klabu ambazo zipo tayari kupata huduma ya kinda huyo aliyesaini mkataba mpya klabuni Chelsea wa miaka mitano.
Lakini kuna taarifa zinadai Musonda Jr mwenyewe anataka kurudi Real Betis ya Hispania ambayo aliichezea kwa mkopo msimu uliopita kabla ya kurudishwa na kocha Antonio Conte kwenye dirisha dogo la mwezi januari mwaka jana.
Kuna taarifa kuwa Chelsea inataka nyota huyo asiende kucheza nje ya Uingereza ili apate uzoefu zaidi katika soka la nchini hapo.
No comments:
Post a Comment