Joe Anderson ambaye ni meya wa jiji la Liverpool nchini Uingereza amepokea majibu ya barua yake aliyowaandikia polisi wa jijini kwake juu ya wasiwasi wake kwa usajili wa kiungo nyota Ross Barkley aliyesajiliwa na Chelsea kutokea klabuni Everton, ambayo inapatikana kwenye jiji lake.
Meya huyo aliandika ujumbe kuupeleka kwa polisi ili kufanyia uchunguzi usajili wa Barkley akihisi huenda kuna udanganyifu ulifanyika kwenye usajili huo mara baada ya kabla kutangazwa nyota huyo atatua Chelsea kwa dau la paundi milioni 35 lakini baadae kidogo wakati nyota huyo ashatangazwa rasmi kuwa nyota wa Chelsea ikatangazwa amesajiliwa kwa paundi milioni 15.
"Tumefanya uchunguzi juu ya usajili wa Ross Barkley na hatujaona aina yoyote ya udanganyifu. Lakini tumeiandikia barua FA ili nao wakigundua kama kuna udanganyifu basi watujulishe" ni ujumbe ulioandikwa na afisa wa polisi Serena Kennedy kwenda kwa meya huyo.
Kutokana na wasiwasi wake akaamua kuandika barua kupeleka polisi, chama cha soka cha Uingereza(FA) na akapeleka barua kwenye uongozi wa ligi kuu ili ufanyike uchunguzi.
No comments:
Post a Comment