Nyota wa Chelsea ambaye ni raia wa nchini Ghana, Baba Rahman amekamilisha usajili wa kujiunga kwa mkopo tena na klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani, inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga.
Rahman mwenye miaka amejiunga tena na klabu hiyo ambayo aliichezea klabu hiyo mwanzo akitokea Chelsea kwa mkopo ambapo huko hakucheza muda mrefu na kupata majeruhi yaliyomfanya kukaa nje karibu msimu mzima.
Kuondoka kwa nyota huyo anayecheza kama mlinzi wa kushoto kunamaanisha Chelsea inabakiwa na mlinzi wa kushoto mmoja tu ambaye ni Marcos Alonso huku Kennedy nae akijiunga kwa mkopo na Newcastle.
No comments:
Post a Comment