HUDSON-ODOI; NINA FURAHA KUWA HAPA - Darajani 1905

HUDSON-ODOI; NINA FURAHA KUWA HAPA

Share This

Alikuwa Chelsea toka mwaka 2007, akijiunga akiwa kama mmoja wa wachezaji chipukizi wenye kipaji cha hali ya juu klabuni Chelsea huku jana akiichezea mchezo wa kwanza kwa timu ya wakubwa akiingia kuchukua nafasi ya Pedro Rodriguez katika dakika ya 80.

Anaitwa Callum James Hudson-Odoi ambapo kwa sasa ni mchezaji anayetazamwa kufanya makubwa huku kwa sasa akiwa na miaka 17 lakini akiwa amehusika kwenye timu ya taifa ya chini ya miaka 17 kwa vijana wa Uingereza na kuisaidia timu hiyo kushinda taji moja la dunia kwa umri huo, lakini pia kufika fainali ya michuano ya Ulaya kwa timu za taifa.

Mara baada ya kuichezea Chelsea mchezo wake wa kwanza hapo jana, nyota huyo alihojiwa na kusema "Kiukweli nina furaha sana kuichezea Chelsea. Nimekuwa na kulelewa hapa tangu nikiwa na miaka nane na nimekuwa vyema nikiwa hapa. Nimefurahi kucheza mchezo wangu wa kwanza"

"Kocha ameonyesha kuniamini na kunipa nafasi. Nilikuwa na furaha sana. Kiukweli lilikuwa jambo zuri. Nimekuwa nikifanya mazoezi na kikosi cha kwanza mara nyingi na najihisi napata kujiamini sana katika hilo. Mchezo dhidi ya Newcastle (Uliochezwa jana) ulikuwa ni mchezo mzuri kwangu ingawa sio wa mwisho, kwa maana hiyo natakiwa kuwa na bidii zaidi ili niweze kupata nafasi zaidi na ni jambo zuri kuona wazaliwa na wachezaji kutokea kwenye akademi wakipata nafasi zaidi" alisema nyota huyo.

Callum Hudson-Odoi ni mmoja ya wachezaji nyota waliolelewa na kukulia kwenye akademi ya Chelsea na kutokea huko wamekuwa ni nyota ambao baadhi wametolewa kwa mkopo na wengine kuuzwa kabisa.

No comments:

Post a Comment