CONTE AWAPA SOMO BODI YA CHELSEA - Darajani 1905

CONTE AWAPA SOMO BODI YA CHELSEA

Share This

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amekuwa akihojiwa na kuulizwa juu ya hatma yake klabuni Chelsea na mara zote amekuwa akisema hatazamii kuondoka klabuni hapo ifikapo mwisho wa msimu kama inavyoripotiwa na vyombo vingi vya habari vikidai kuwa kocha huyo hana furaha klabuni hapo huku sababu kubwa inayotajwa kumfanya kutokuwa na furaha ni jinsi mfumo wa usajili ulivyo klabuni Chelsea ikielezwa kuwa kocha ana nafasi ndogo ya kufanya usajili kutokana na mapungufu na mahitaji ya kikosi.

Kutokana na hilo na mfululizo wa matokeo mabaya ambayo Chelsea imeyapata katika michezo kadhaa huku ikishinda michezo miwili kati ya 10, kumesababisha kuchochea kwa fununu za kocha huyo kuondoka Chelsea huku bodi ya klabu hiyo ikiongozwa na mwanamama Marina Glanovskaia ikitajwa kwa karibu kuachana na kocha huyo, kocha huyo ameibuka na kutoa kauli juu ya kinachoendelea kwa sasa.

"Ili umtimue kocha, mtimue kutokana na kutokumuamini, sio kwa vile hajasaidia timu ibebe makombe, maana sio rahisi kushinda taji, haswa kwa hapa Uingereza." alisema kocha huyo raia wa Italia mwenye miaka 47 kwa sasa.

"Kama hauna imani na kocha, basi hapo ndio inatakiwa umwambie sasa anaweza kwenda, na sio kumfukuza kisa kubeba kombe. Kuna wangapi hawaaminiki na timu na wanabeba makombe lakini mwisho wa siku wanatimuliwa?" alisema kocha huyo ambaye msimu uliopita aliisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu Uingereza.

Chelsea kesho itakuwa nyumbani kupambana dhidi ya West Bromwich ambapo itahitaji ushindi ili ijiweke katika nafasi nzuri ya kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao, lakini pia utakuwa mchezo muhimu kwa Antonio Conte kutaka kupata ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea kubaki Chelsea mpaka mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu wa 2018-2019.

No comments:

Post a Comment