DI MATTEO ANAPONOGESHA UTAMU WA MECHI YA LEO - Darajani 1905

DI MATTEO ANAPONOGESHA UTAMU WA MECHI YA LEO

Share This
Nimekuwa nikikuletea mfululizo wa walichokifanya mashabiki wa Chelsea siku Chelsea walipotawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ulayakatika michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa mwaka 2012 ambapo fainali hizo zilichezwa huko jijini Munich na wenyeji wa jiji hilo, Bayern Munich tena katika uwanja wao wa Allianz Arena ambao pia umekuwa ukitumiwa na timu ya taifa ya nchi hiyo, Ujerumani kama uwanja wao mwenyeji. Kama unahitaji kuyapata matukio hayo, bonyeza hapa

Sasa nadhani unakumbuka, kocha wa Chelsea wakipindi iko alikuwa muitalia, Roberto di Matteo ambaye alishawai kucheza Chelsea toka mwaka 1996 mpaka mwaka 2002 na kuja kuwa kocha wa Chelsea akichukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa Chelsea wa kipindi iko, Andre Villas Boas.

Sasa nataka nikujuze jambo ambalo huenda hulijiui kuhusu kocha huyo ambaye kwa sasa hana timu. Je unajua kama kocha huyo alishawai kuifundisha klabu itakayokuwa uwanjani usiku wa leo kupambana na Chelsea? namaanisha West Bromwich.

Ipo hivi mara baada ya kustaafu soka mwaka 2002 akistaafu mara baada ya kuachana na Chelsea alipoichezea michezo 119 na kuifungia magoli 26, akaingia kwenye fani ya ukocha na hapohapo akaanza kuifundisha klabu ya nchini Uingereza, MK Dons aliyoifundisha miaka sita mara baada ya kustaafu ambapo sababu kubwa ya kustaafu kwake ilikuwa kutokana na majeruhi huku akistaafu akiwa na miaka 31 tu, yaani kama leo kwa umri wa Cesc Fabregas aamue kuachana na soka.

Baada ya kuifundisha MK Dons, mwaka mmoja baadae, nazungumzia mwaka 2009 akaungana na West Bromwich, ambapo alikuwa hapo kwa akiteuliwa mara baada ya klabu hiyo kushuka darajja kutoka ligi kuu mpaka kufikia kwenye oligi daraja la kwanza maarufu kama Championship.
Roberto Di Matteo akiwa kama kocha wa Chelsea

Lakini kutokana na ubora wake alipambana na kufanikiwa kuirudisha ligi kuu klabu hiyo wanaojiita The Baggies kama jina la utani ndani ya msimu huohuo wakimaliza nafasi ya pili katika ligi hiyo huku wakifanikiwa kupanda wakiwa na michezo mitatu mkononi.

Baada ya kufika ligi kuu, aliendelea kuwa kocha wa West Brom na alifanikiwa pia kurudi tena Stamford Bridge ambapo klabu yake ilifika uwanjani hapo kumenyana dhidi ya Chelsea iliyokuwa na ubora mkubwa na wachezaji kama Didier Drogba, Michael Essien, Florent Malouda, Nicolas Anelka na Frank Lampard, ambapo hiyo ilikuwa mwaka 2009 na mashabiki wa Chelsea walimpokea vyema na kufurahishwa na ujio wa mchezaji wao wa zamani ambaye kwa muda huo alikuwa kama kocha wa Chelsea, Chelsea aliyokutana nayo hapo haikuwa ya mchezo kabisa maana mpaka mpira unaisha, alishakufa kwa mabao 6-0 huku Didier Drogba akifunga magoli matatu, Malouda akifunga mawili na jengine akifunga Frank Lampard. Lakini kwa msimu huo aliinusulu na kufanikiwa kumaliza nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi kuu.
Roberto Di Matteo alipokuwa kocha wa West Bromwich

Tarehe 29-Juni-2011, Di Matteo akatangazwa rasmi kuwa kocha msaidizi wa Chelsea na alikuwa kwenye nafasi hiyo mpaka mwezi Marchi-2012, alipochaguliwa kuwa kocha wa muda wa Chelsea mara baada ya kocha mkuu, Andre Villas Boas kuwa na matokeo mabovu, na toka kuanzia hapo akaisaidia Chelsea kuwa klabu ya kwanza katika jiji la London, jiji lenye klabu nyingi za mpira pale Uingereza kubeba taji la ligi ya mabingwa Ulaya, lakini pia akaisaidia kushinda kombe la FA mara baada ya kupata ushindi dhidi ya Liverpumba (Liverpool).
Roberto Di Matteo mara baada ya kuiongoza Chelsea kushinda UEFA mwak 2012

Kwa maana hiyo mchezo wa leo unazihusisha timu ambazo zimewai kupata furaha chini ya kocha mmoja raia wa Italia mwenye asili ya Switzerland, Roberto Di Matteo ambapo kwa upande wa West Bromwich walipanda daraja kutoka Championship mpaka ligi kuu chini ya kocha huyu wakati kwa upande wa Chelsea ilipata taji lake kubwa la kwanza la klabu bingwa Ulaya chini ya muitaliano huyu.
Roberto Di Matteo akiwa na Gianfranco Zola pindi walipokuwa Chelsea

No comments:

Post a Comment