Chelsea lo itakuwa uwanjani kupambana dhidi ya West Brom, mchezo utakaochezwa kwa raundi ya 27 ya ligi kuu Uingereza ambapo Chelsea itahitaji kupata ushindi wake wa kwanza mara baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo, kama ikifanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa leo, basi itafanikiwa kupata alama tatu zitakazoipandisha kutoka nafasi ya tano ilipo kwa sasa mpaka nafasi ya nne ambapo nafasi hiyo inashikiriwa na Tottenham ambao wamefika kwenye nafasi hiyo mara baada ya kuibamiza Arsenyani (Arsenal)
Hapa nakuletea habari muhimu kuelekea mchezo huo wa leo usiku.
Habari muhimu;
Chelsea; Alvaro Morata na Andreas Christensen wataendelea kuwa nje licha ya Christensen kuanza mazoezi japo siyo ya jumla na wenzake, lakini pia Tiemoue Bakayoko atakuwa nje kutumikia adhabu yake ya kukosa mchezo mmoja mara baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano katika mchezo uliopita dhidi ya Watford, Ross barkley naye pia ataendelea kuwa nje. Lakini inatazamiwa kwa upande wa Olivier Giroud anaweza kutumika kama mshambuliaji wa kati kutokana na kuhitajika mchezaji anayecheza namba tisa kiasili.
West Bromwich; Johhny Evans, Kieran Gibbs, Grzegorz Krychowiak, na Jay Rodriguez watapatikana katika mchezo wa leo mara baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na majeruhi lakini nyota kama Jake Livermore, James Morrison na Nacer Chadli watakuwa nje kutokana na majeruhi.
Mwamuzi; Lee Mason, kwa sasa ana miaka 47 na tayari ameshachezesha michezo 17 kwa msimu huu wa 2017-2018 huku akitoa kadi 46 za njano na kadi nyekundu tatu nyekundu. Ambapo kwa msimu uliopita alichezesha michezo 25 na kuonyesha kadi 96 za njano na kadi nyekundu 3.
Rekodi; Chelsea tangu ikiwa chini ya kocha Antonio Conte haijawai kupata ushindi wowote huku ikishindwa kupata goli hata moja lakini pia katika michezo 16 ambayo Chelsea imecheza dhidi ya West Brom katika uwanja wa Stamford Bridge ambapo Chelsea imeshinda michezo 13 na kutoa suluhu michezo mitatu ambapo mara ya mwisho kwa Chelsea kupoteza katika uwanja huo ilikuwa mwaka 1983.
Mchezo uliopita; West Bromwich 0-4 Chelsea
Michezo iliyopita;
Chelsea; WLWLL
West Bromwich; WDWLL
Muda; Saa 11:00 usiku (saa 23:00) kwa saa za Afrika Mashariki
HABARI MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs WEST BROMWICH
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment