HERI YA KUZALIWA MAKELELE - Darajani 1905

HERI YA KUZALIWA MAKELELE

Share This

Chelsea ilimtangaza rasmi kiungo raia wa Ufaransa, Claude Makelele mwaka 2003 ambapo alifika hapo na kuwa moja ya viungo ngangari na imara kuwai kutokea klabuni Chelsea na hata nchini kwao Ufaransa. Alikuwa ni nyota wa timu aliyehakikisha usalama katika eneo la ulinzi la klabu.

Kwa Chelsea yake aliyocheza, aliisababisha timu hiyo kuweka rekodi nyingi na nzuri akisababisha Chelsea kushinda taji la ligi kuu huku Chelsea ikiruhusu magoli machache kwa msimu mzima mpaka alipoondoka mwaka 2008 na kuacha rekodi klabuni hapo na nchini Uingereza.

Leo nyota huyo ambaye anafanya kazi ya ukocha nchini Ubelgiji ambapo huko anafanya kazi kama kocha mkuu mara baada ya kutoka Swansea ambapo alikuwa kocha msaidizi kwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwa kipindi iko, Paul Clement ambaye baadae alitimuliwa.

Jambo usilolijua kuhusu Makelele, kiasili alizaliwa nchi ya Demokrasia ya Kongo inayoitwa hivyo kwa miaka ya leo na alizaliwa kwenye familia ya soka ambapo baba yake alikuwa nyota mpaka kucheza nchini Ubelgiji.

Alicheza Chelsea kwa michezo 144 huku akiisaidia kutwaa mataji yote ya Uingereza ambapo Chelsea ilishinda mataji ya ligi kuu Uingereza, Kombe la FA, kombe la ligi  na ngao ya hisani nchini umo.

Heri ya kuzaliwa Makelele, miaka 45

1 comment:

  1. The keyword cricbet99 zimbabwe t20 betting can be relevant for users following Zimbabwe in T20 cricket and looking for event-related information. T20 matches often develop quickly, making current team news, player form, pitch conditions, and recent results useful for understanding the contest. Users should review the relevant terms and applicable restrictions before participating in any related activity. Responsible engagement is important, particularly during live matches. Following the sport carefully and using reliable information can help create a more informed cricket experience.

    ReplyDelete